Shakti Women's Aid

Shakti ni charity inayo toa huduma kwa wanawake na watoto kutoka Ethnic Minority wanao kimbililia usalama kutokana na mateso wanayo pata kutoka kwa mume, mpenzi, mume wa zamani walio tengana ama familia.

We we ni moja ama wamjua anaye chapwa?
Kusukumwa ama kuchapwa tege?
Kuwekwa chini?
Kutukanwa vibaya?
Kuongopeswa?
Kulazimisha kufanya mapenzi?
Kutiwa rumande?
Kukataliwa kuona familia ama marafiki?
Wasiwasi kulazimishwa ndoa?
Watu wanao ishi nawewe wana kutenda vibaya?
Kutishwa kurudishwa inchi yako ama kuaribiwa makao yako?

Kama hii ina kutokea ama mtu mwingine unaye mjua, unaweza kupokea msaada kutoka kwetu. Ni haki yako kusikia na kuwa salama.

Kama wewe una patwa na matatizo ya kutujanwa ama kuchapwa, usiongope kupokea msaada unaw eza kupigia Shakti simu, unaweza pia kuongea na Dactari wako, health visitor na Social worker kwa siri.

Shakti Inatoa vyumba salama vyakukaa kwa mda mchache, maelezo ya sheria, benefiti, kazi nakadhalika na pia wakati wa matikira.

Unaweza kupokea msaada wa wanawake na watoto, kama unaishi inje ya mji wa Edinburgh nab ado unafikiria kutengana na mume wako na familia, fuata usaidizi wawanawake na watoto waliyo wacha kimbililio ama makao ya refuge.

Wafanyi kazi wa Shakti wanaongea zaidi ya lugh a ishirini, kingereza pia.

Piga simu kwa 0131 475 2399 tunafungua kutoka Jumaatatu mapaka Ijumaa saa tatu na nusu asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.

Kumbuka kama uko kwa hatari tafadhali piga tisa tisa tisa (999).

Unaweza pia kupiga kwa Scottish National Domestic Abuse Helpline kwa 0800 027 1234 inapatikana masaa ishirini na ine.

Polisi na National Domestic Abuse Helpline wana weza kutoa mtafsiri

Kiswahili
BSL info on Forced Marriage (Ishara Project)
info@shaktiedinburgh.co.uk
Copyright 2009. Shakti Women's Aid. All rights reserved | Registered Scottish Charity Number SC008837
Shakti Women's Aid is a company limited by guarantee, Registration Number SC273279 | Design by Creative Link
Arabic
Polski
Español
Português
Gaidhlig